Burudani

Q Boy Msafi apata shavu la show za kimataifa

By  | 

Msanii wa muziki, Q Boy Msafi ameanza maandalizi ya tour yake ya kimaitafa ikiwa ni miezi kadhaa toka aingie rasmi kwenye muziki akitokea kwenye masuala ya fashion.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Karorero’, hivi karibuni alikuwa kwenye BBM Tour ya Young Dee iliyoandaliwa na King Cash pamoja na Mabula Entertainment, amesema tour hiyo imeweza kumzalishia show mbalimbali.

“Kusema kweli namshukuru sana Mungu mambo yanaenda vizuri sana, tour ya BBM imezaa matunda sana, wadau wengi wananipigia simu kutaka show kwahiyo kwangu naona huu ni mwanzo mzuri wa muziki wangu na kwenda mbali zaidi,” alisema Q Boy.

Aliongeza, “Tayari kuna show za kimataifa zimeanza kuja, ni nyingi na mungu akipenda zitakuwa nyingi zaidi kwa sababu bado kuna watu nazungumza nao kuhusu show. Lakini yote kwa yote naomba ushirikiano kwa mashabiki wangu ambao walikuwa na mimi kwa muda mrefu, wadau wa muziki pamoja na wasanii wenzangu,”

Muimbaji huyo ambaye alikuwa stylish ya Diamond, aliachana na Kazi hiyo na kuamua kufanya muziki kwa kuwa ndio plan yake ya muda mrefu.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments