Burudani

Q Chief adai hataki kukurupuka kusaini label yoyote

Ikiwa ni miezi 3 toka msaniii wa muziki, Q Chief aachanae na label yake ya zamani, QS J Mhonda Entertainment, bado hajasaini mkataba na label yoyote.

Q Chief akiwa na bosi wake wa zamani, QS Mhonda.

Muimbaji huyo ambaye anajipanga kuachia wimbo wake mpya hivi karibuni, ameiamba Bongo5 kwamba, hataki kukurupuka kusaini mkataba na label yoyote.

“Namshukuru Mungu mambo yanaenda vizuri nikiwa nje ya label,” alisema Q Chief. “Label nyingi niko nazo kwenye mazungumzo na namshukuru Mungu mambo yanaenda vizuri na kikubwa zaidi sitaki kukurupuka kusaini label yoyote tu halafu baadae nijutie,”

Aliongeza, “Kama unavyoona bado niko peke yangu, pamoja na watu wangu wa karibu ambao wananisaidia lakini mambo yanaenda. Kuna label nyingine iliniambia nifanye kazi kwanza halafu tuone mambo yatakuwaje,”

WCB ya Diamond ni moja kati ya label ambazo zilionyesha dalili za kumchukua muimbaji huyo mkongwe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents