Q Chief akiri alikuwa akitumia madawa ya kulevya, asema ‘I am responsible for my failure’

qchilla

Muimbaji Abubakar Katwila aka Q Chief amekiri kuwa alikuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya kwa kipindi cha miaka miwili na hivyo kumharibia maisha yake.

Hata hivyo amesema amefanikiwa kuacha kutumia miezi saba iliyopita baada ya kutumia muda mwingi kufanya ibada.

Akiongea kwa uchungu katika mahojiano exclusive na kipindi cha XXL cha Clouds FM, Chilla amesema hakuweza kusema wazi jambo hilo kwakuwa aliogopa kuwaumiza watu zaidi.

“Nilifikiria kwanza kabla ya kuconfess kwamba hata nikiconfess I know there are a lot of people who care about Q Chief na wasingependa kumuona yuko hapa katika hali hii lakini pengine ukawaamiza zaidi,” alisema.

“Nimepitia mambo mengi katika maisha yangu lakini I don’t want to blame anyone, I wanna be responsible for my own failure.”

Japo alikataa kusema, Q alisema kitu kingine kikubwa zaidi ya madawa ya kulevya kilichompelekea yeye kufika hapo alipokuwa.

Kupitia mahojiano hayo Q Chief ametambulisha wimbo wake mpya uitwao Butterfly.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents