DStv Inogilee!

Q Chief amtoa machozi muimbaji Nuru Light

Mahojiano ya msanii Q Chief na mtandao wa Bongo5 kuhusu maisha yake na tamko lake la kutaka kuacha muziki, limekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii.

Mashabiki wengi katika mitandao ya kijamii wamekuwa na huruma na muimbaji huyo huku baadhi ya wasanii akiwemo, Nuru Light akiandika ujumbe mzito juu ya masikitiko yake.

Nuru aliandika ujumbe huu…

Naandika this with heavy heart.Jana usiku sana nimeona interview mbili tofauti na Q Chief maisha yake kwasasa na Changamoto anazopitia. HE Spoke Very open na kwa unyenyekevu kuhusu kuacha MZIKI. INDUSTRY YA MZIKI INA SIRI NYINGI NA CHANGAMOTO NYINGI SANA. INDUSTRY hii INA watu wazuri na Wabaya Pia.

Q imeniuma kuwa unajiona huwezi au unakosea wakati you are The Real talent kwani Industry yetu inawatu wanaoweza kukufanya uonekane huwezi au uangamie kabisa na nimesikitishwa kuwa They took one of The best.Umekiri ulikosea kwa kutumia madawa na kuacha tuna wasanii wakubwa kwenye kila tasnia ndani na nje wanaotumia na walitumia na bado wanafanya shughuli zao vizuri tu.Your misstake should not define you or Your talent.

Q bado nafasi yako ipo na bado uwezo unao.Nyie ndio mliopigania huu MZIKI sasa kwanini Leo hii msile yale matunda.Kuanzisha kitu na kukipigania na kuonwa kizuri sio kazi ndogo kabisa naomba mjivunie hilo wasanii wa zamani na hata wajinga pumbavu mashabiki wakiwatukana kwa kutumia maneno YA umefulia,zilipendwa dont ever feel that kwani kazi mloifanya ni kubwa mnaijua kuliko anybody else.Ningependa ujue kutoka kwangu mie that I love you, I appreciate you, Respect you vilevile natambua nafasi yako kwenye MZIKI wa Bongoflava.

My People Q anatuhitaji sisi more than ever let US support kazi yake mpya Saratani akiitoa cause inawezekana kuwa his last!

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW