Tupo Nawe

Q Chief arudi kuomba msamaha kwenye kampuni ya QS Mhonda

Baada ya msanii wa Bongo fleva Abubakar Katwila a.k.a Q Chief kutangaza kujiondoa kwenye usimamizi wa kampuni ya Q S Mhonda, hatimaye muimbaji huyo na kampuni hiyo wamemaliza tofauti zao baada ya kukutana na kufanya mazungumzo.

Q Chief

Mkurugenzi wa kampuni hiyo bwana Mhonda amesema kuwa wakati Q Chief anatangaza uamuzi wa kujiondoa kwenye kampuni yake hakuwepo jijini Dar, hivyo aliporejea Chilla aliomba kuonana naye ili kutafuta suluhisho.

“Ofcoz tulikutanakumbuka na mimi nilikuwa naendelea na shughuli zangu, nikapata ujumbe kwamba aliomba tuonane nae…nikawa nimekutana nae” alisema Mhonda kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm.

Baada ya Mhonda kukutana na Chilla amesema aligundua kulikuwa na misunderstandings tu kwa pande zote mbili ambazo waliweza kuziweka sawa.

“Nilichogundua baadae ni kwamba kulikuwa na misunderstandings, unajua vitu wakati vimetokea mimi nilikuwa siko Dar es salaam nilikuwa niko mikoani…kwahiyo kuna vitu ambavyo yeye alihisi viko hivyo kumbe ndivyo sivyo. Sasa wakati tulipokutana alikuja politely si vile ambavyo nilikuwa nimetarajia kama alivyokuwa ameongea kwenye redio.” Alieleza Mhonda.

“Nikajaribu kumweleza kile ambacho mimi nakifahamu, kwahiyo ikaonekana kwamba kumbe yeye alielewa tofauti, na mimi pia nilivyosikia redioni sikuweza kumwelewa kwa haraka kwanini ameweza kutokea kwenye media na kuongea vitu vya namna hiyo.” Aliongeza Mhonda.

Baada ya mazungumzo yao Mhonda amesema muafaka uliweza kupatikana na kumsamehe Q Chief kwa yaliyotokea.

“Kwahiyo mwisho wa siku tumeyamaliza kwangu mimi sina kinyongo nimemsamehe, unajua katika hali ya kawaida huwezi ukaendelea kukaa na kitu au unaweza usije ukaacha kumsamehe mtu wakati hata kwenye vitabu vya dini tunafundishwa kusameheana.” Alimaliza Mhonda.

Baada ya taarifa ya Q Chief kujiondoa kwenye kampuni hiyo Bongo 5 ilimtafuta mwanasheria wa kampuni hiyo kutaka kufahamu hatua ambazo wangechukua kisheria kutokana kwamba alikuwa na mikataba nao, ambapo mwanasheria huyo alisema kuwa mkataba ndio ungemhukumu kwani kila kipengele kinaeleza hatua za kuchukuliwa endapo mteja atakiuka taratibu.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW