Burudani

Q-Chief ataja kitu kinachomuumiza zaidi kwenye muziki

Q-Chief amesema katika maisha yake ya muziki aliumizwa zaidi na kushindwa kusamehewa na watu aliowakosea kuliko kupotea kwenye muziki.

chila

Muimbaji huyo ambaye hujulikana pia kwa jina la Q- Chillah, ameiambia Bongo5 kuwa hali hiyo imekuwa sehemu ya kurudi nyuma katika muziki.

“Mimi kiukweli sikuwahi kukata tamaa kwa sababu uwezo wangu nautambua na nina kipaji. Isipokuwa kilichokuwa kinaniumiza ni maswali kwamba kama kuma mtu nimemkosea ni nani asiyeweza kusamehe? Nani huyo ambaye ni Mungu? Na huko ninapokwenda unakutana na Mungu mwingine nitakuwa na hukumu ngapi? Kitu kikubwa nilichofanya ni kurudi kuangalia ni nani ambaye nilimkosea na kuwaambia ‘jamani mimi nina watoto na familia, sauti yangu naiona pesa mbele na utajiri, naomba tumalize tofauti zetu ili maisha yaendelee,” alisema Q.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents