Michezo

Qatar ya husishwa na rushwa kombe la dunia 2022

Ujerumani imechapisha habari inayoelezea namna rushwa ilivyotumika kuipatia nafasi ya kuandaa michuano ya kombe la dunia nchi ya Qatar mwaka 2022.

Gazeti la Bild limesema, ripoti hiyo iliandaliwa tangu mwaka 2014 na kiongozi wa FIFA, Michael Garcia ambaye ni miongoni mwa viongozi waliohusishwa na rushwa katika shirikisho hilo kisha kutangaza kujiuzuru mwezi Disemba mwaka 2014.

Kwa mujibu wa ripoti ya Bild, imejumuisha kitita cha fedha za kimarekani dola milioni mbili (£1.6m) kilicholipwa kwa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 10 wa afisa mmoja wa FIFA.

Mwanasheria wa Marekani aliwahi kuishutumu FIFA kwa kukosa uongozi bora wakati alipoachana na shirikisho hilo, huku viongozi wengine wakichapisha kurasa 42 zenye maelezo ya kukanusha Qatar kuhusika na rushwa katika mchakato wake wa kupata nafasi ya kuandaa michuano hiyo.

Gazeti la Bild limesema linatarajia kuchapisha kurasa 403 zenye maelezo kamili ya Garcia siku ya Jumanne.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents