Qchillah matatani na kesi ya wizi!!

Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Abubakar Shaaban Katwila ’Q-Chillah’,siku ya jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu Dar es Salaam, akikabiliwa na tuhurna za wizi.

Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Abubakar Shaaban Katwila ’Q-Chillah’,siku ya jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu Dar es Salaam, akikabiliwa na tuhurna za wizi.

Q-Chillah ambaye awali alikua akifahamika kwa jina la Q-Chief, alifikishwa kizimbani hapo akikabiliwa na mashtaka mawili la kwanza likiwa ni wizi wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh ml 1.8 na mkwanja taslim sh 906,000 kutoka kwenye gari la msanii mwenzake wa RnB Paul Mbena (Mr Paul),na kosa la pili la wizi wa vifaa mbalimbali vya thamani sh milioni 1.6 mali ya Manispaa ya lIala.

Akisomewa tuhuma hizo na Mwendesha Mashitaka, Inspekta wa Polisi Hudson Ndusyepo mbele ya Hakimu Mkazi, Joachim Tiganga ilidaiwa kwamba, Januari 2 mwaka huu saa 11 jioni Mtaa wa Magore, Upanga jijini Dar es Salaam,
mtuhumiwa aliiba Laptop aina ya IBM, begi moja, Power Window moja, hundi moja, kitambulisho kimoja cha benki ya NBC, viwili vya CRDB na mali mbalimbali kutoka kwenye gari namba T 853 AHE Vitara.

Msanii huyo alikana kosa na kurudishwa lekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamani wawili watakaosaini mkataba wa sh milioni 2 kila mmoja. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Januari 30 itakapotajwa tena.

Katika kesi iliyofuata, ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashitaka kuwa msanii huyo huyo Desemba 30 mwaka jana saa tano usiku..kwenye Ukumbi wa Utamaduni wa Korea uliopo Upanga, Q Chillah aliiba Baskrest nne, Control Box moja na Power Window nne mali ya Manispaa ya IlaIa.

Kaka Qchillah vipi mzee!!! haya yanayosemwa ni kweli au wakusungizia yakheee???

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW