“Nayafurahia maamuzi yangu” Young Buck

Inasemekana lile duku duku la msanii aliyekuwa miongoni mwa wasanii wa kundi la G-Unit, Young Buck, bado limekuwa likimchanganya mchizi huyo ambaye amekuwa akisikika kujutia kwake kuchelewa kuchomoka katika kundi hilo

Young Buck


 


Inasemekana lile duku duku la msanii wa muziki wa Hip Hop na aliyekuwa miongoni mwa wasanii wa kundi la G-Unit, Young Buck, bado limekuwa likimchanganya mchizi huyo ambaye mpaka sasa amekuwa akisikika kujutia kwake kuchelewa kuchomoka katika kundi hilo na utawala wa mheshimiwa Curtis Jackson a.k.a 50 Cent.



“Tangu nimesaini na 50 hajawahi hata siku moja kufika nyumbani kwangu, hajui hata ninapoishi na familia yangu, pia sidhani hata kama analijua jina la mtoto wangu wa kwanza na wa mwisho sasa huyo ni rafiki kweli?” Alisikika akihoji mtu mzima Young Buck ambaye hivi karibuni mkali huyo ilitangazwa rasmi kutokuwepo katika kundi la G-Unit.



Buck alisikika akizungumza katika moja ya kituo cha redio cha MX Radio huko marekani ambapo alisema kuwa “ni mambo mengi ambayo 50 Cent ameyafanya katika hali ambayo imenifanya niwe natumika pasipo kuangalia maisha yangu ya mbele, nimekuwa kama niko jela kwa kipindi kirefu sana mpaka kufikia hii leo nimekuwa na msimamo na maamuzi yangu ambayo nayafurahia kwani nikiwa chini ya 50 sijawahi kuwa mwenye furaha hivi na ninaamini kipaji changu hakidanganyi kwani niko fiti ile mbaya”.



Aliendelea kusema “ kipindi ambacho 50 alitangaza kuwa sipo tena katika kundi la G-Unit, Meneja wangu ambaye pia ni rafiki yake, ajulikanaye kwa jina la Sha Money sikuweza kuonana nae kwa kipindi cha wiki mbili tatu, bila ya kuwa na mawasiliano nae lakini baada ya yote haya kutokea niliendelea kumpigia simu lakini sikumpata, kitu nachoweza kusema kama japo Sha ndio Meneja wangu pia ni mchizi wangu kwani nimekuwa nae halikadhalika nilikuwa ni best man wake siku ya harusi hivyo naamini kufanya nae mengi tu ya maendeleo.


 



 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents