Burudani

Queen Darleen afungua ndoa kimya kimya na mfanyabiashara huyu ? (Picha)

Mwanamuziki Queen Darleen amefunga ndoa kimya kimya na mfanyabiashara wa magari jijini Dar es salaam.

Muimbaji huyo ambaye yupo chini ya WCB, amefunga ndoa siku ya jana na kuhudhuriwa na ndugu jamaa na marafiki.

Kwa mujibu wa picha ambazo zimesambaa mitandaoni zinadai kwamba mfanyabiashara hiyo anaitwa Isihaka.

“Sijui nilie jana nimekosa ila tunairudia hongera sana ndugu yangu dadaangu Mungu akubariki ktk ndoa yako akuepushe na husda za walimwengi yani daah Mungu ni mwema shem langu nakupenda sina cha kusema Wallah @queendarleen_ jishebedue wakuone 👌 ridhiki mafungu saba,” alindika Esma tupitia Instagram.

Wadau wa mambo wanadai huwenda hiyo isiwe ndoa kwani, kwani mwanaume huyo ambaye ameonekana kwenye picha hapo juu ni mume wa watu.

Je wewe unadhani ni ndoa kweli au kuna project inakuja.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents