Burudani

Queen Darleen: Sina kinyongo na mawifi zangu kwa Diamond

Queen Darleen ambaye ni dada yake na Diamond, hana tatizo na ‘bandika bandua’ ya mawifi wanaotambulishwa kwake na kaka yake huyo. Kwa mujibu wa Queen, hayo ni maisha yake na anayaheshimu.

diamond queen darleen

Queen ambaye pia ni mwanamuziki, amesema kila msichana anayetambulishwa kama wifi yake, humpa heshima anayostahili.

“Mapenzi siku zote ni ya watu wawili ndio maana unaona hata mimi nina maisha yangu kama maisha yangu siingilii chochote. Yaani mimi Diamond ukitaka kunichafua umwongelee vibaya. Jambo lolote baya kuhusu yeye, muziki yake na maisha yake binafsi. Kwa sababu kuna watu wengine wanapenda kuzungumzia mambo ya watu, ‘sijui Diamond anaringa’,” ameiambia Bongo5.

“Mimi ni ndugu yake na ninamjua Diamond kwahiyo tutagombana kwaajili ya kukusahihisha, siwezi kumuingilia Diamond katika mahusiano yake, sijui yuko na huyu leo yupo na yule! mimi haiwezi kuniuma kwa sababu mimi najua yeye anachagua kilichokuwa bora. Mimi nachohitaji nimuone mdogo wangu ana furaha na yupo kwenye amani basi! Mwanamke yoyote atakayeamua kuwa naye yeye kwa sababu mimi mwenyewe mapenzi nayajua. Kwahiyo mpenzi yoyote atayekuwa naye Nasib atakayenitambulisha kwamba ‘huyu ni mwanamke wangu’ na mimi nikafahamiana naye basi nitamuheshimu, na hata wakiachana siwezi kuingilia chochote.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents