Burudani

Quick Rocka amkumbuka Ngwea, ‘tutaendelea kuenzi alichofanya’  

Msanii wa Bongo Flava, Quick Rocka amesema pengo la Marehemu Ngwea bado linaonekana katika muziki.

Katika mahojiano na Bongo5 Quick Rocka amesema kutokana na hilo kuna vitu anavikosa katika muziki wake na tasnia nzima, hivyo akatoa wito kwa Watanzania kujijengea utamaduni wa kuthamini wasanii pindi wangali hai.

“Naweza nikawa studio tumepiga ngoma nasikiliza nasema angekuwepo bro Ngwea angeua hii ngoma, we still miss him, tunaoana bado tunamuhitaji na kama alivvyosema pengo lake halina spare hamana hata spare moja imeweza kuziba, so we still appreciate what he did na tutaendelea kuenzi kazi alizofanya,” amesema Quick.

“Kikubwa nachoweza kusema kwa watanzania tuheshimu sana wasanii wetu kwa sababu pindi wanapoondoka ndio tunajua umuhimu wao. Ujue sisi tumejitoa kufanya muziki, kusapoti watu wengine kama hivi lakini tunaweza tusifaidi sana, vikaja kufaidika vizazi,” ameongeza.

Quick Rocka alimshirikisha Ngwea katika ngoma yake ‘My Baby’ ambayo pia alikuwepo Shaa. Pia walikutana kwa pamoja katika ngoma ya Izzo Bizness ‘Ball Player’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents