BurudaniHabari

“Usiulize” Rado akidiss wasanii wenzake

RadoMsanii Rado ambaye hapo miaka ya nyuma aliwahi kutamba na singo yake ‘hukumu ya ndotoni’ hivi sasa ametoka na singo yake mpya ambayo ndani yake amewadiss wasanii kama Fid Q na Kundi zima la East Coast inayokwenda kwa jina la ‘usiulize’. [Sikiliza Singo hapa!!]

RadoMsanii Rado ambaye hapo miaka ya nyuma aliwahi kutamba na singo yake ‘hukumu ya ndotoni’ hivi sasa ametoka na singo yake mpya ambayo ndani yake amewadiss wasanii kama Fid Q na Kundi zima la East Coast inayokwenda kwa jina la ‘usiulize’.

“Nimewadiss jamaa makusudi kwani nina sababu za msingi za kufanya hivi, sababu ya kumdiss Fid Q ni kwa sababu anajifanya anawakilisha Hip Hop wakati ameniibia mistari yangu na kuitumia katika wimbo wake wa ‘mwanza mwanza’ nayo ni ‘sio kila ndio ina undio kiundani ndio bali kuna baadhi ya ndio zimeambatana na utani’

Aliendelea kusema Rado “kuhusu hawa East Coast Team wanakuwa wanaandika tungo ambazo wao wenyewe wanakuwa hawajui wanamaanisha nini kama ndio maana katika singo langu nikawaambia kuwa ‘Ama zangu ama zao walisema bila upeo nauhofia uwezo wao na sasa ndio ama zao’ nadhani hii itasaidia kupata wasanii ambao watakuwa ni halisi na hawafanyi mambo kwa kuigiza na kuonekana tu”

Rado ambaye kwa sasa ngoma yake hiyo imekuwa ni gumzo hapa jijini, yuko katika harakati za kukamilisha albam yake ambayo itakuwa mitaani muda si mrefu na alichosisitiza ni kuwa “wasanii wawe wa kweli na sio kuwa wababaishaji kama Fid alikuwa ni mchizi wangu sana lakini nimeshangaa sana jamaa kuchukua jukumu la kuniibia mistari jambo ambalo hata yeye mwenyewe anaamini alichofanya si sahihi, hivyo lengo langu ni kumtaka ajue na asirudie tena kufanya hivyo kwani hip hop daima ni ukweli na sio kuzuga mashabiki”

SIKILIZA SINGO “USIULIZE” YA RADO
{play}rado_usiulize.mp3{/play}

Source: Bongo5

{mos_sb_discuss:6}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents