Burudani

R Dj Mamie wa E-Fm awachana ma-dj wa kike

Dj pekee wa kike ambaye anafanya vizuri kupitia E Fm Radio,  R Dj Mamie amewachana baadhi ya ma-dj wa kike ambao wanaamini katika uzuri wao ili kupata kazi na si uwezo.

“Sisi wadada tunashindwa kujiamini, kwa mfano mimi ni dj mkali, najua in short, mimi najua siyo kwamba nabahatisha, kipaji changu ndio kimenifanya nimefika E Fm sijatumia njia yoyote ya ziada kusema labda nilifanya hivi na vile kwa sababu ujue pia boss wetu ni dj, kwa hiyo wewe ukiwa kama ni dj halafu wa kubahatisha anakujua dakika sifuri” amesema.

“Kwa hiyo mimi ni dj mkali najua ndio maana nimefika hapa nilipo kwa hao ambao wanatumia vigezo kwamba ni washichana, wanatumia uzuri wao ili wapate kazi naona kama hawajielewi” R Dj Mamie ameiambia Bongo5.

Katika hatua nyingine ameeleza kuwa licha ma-dj kuchukuliwa kama watu wa kawaida katika music industry ya Tanzania, malengo yake ni kufanya vizuri na siku moja kuwakilisha nchi katika mashindano/tuzo kubwa za u-dj nje ya nchi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents