Tupo Nawe

R Kelly ahofia Virusi vya Corona ndani ya Gerezani, aomba kuachiwa huru

Msanii wa muziki wa R&B, nchini Marekani Robert Kelly maarufu kama R Kelly amemuomba jaji kumuachia huru kutoka katika Gereza la Metropolitan Correctional Center huko Chicago akihofia kupata maambukizi ya ugonjwa Virusai vya Corona.

Hivi karibuni majaji wa mahakama za Chicago walionyesha nia ya kumuachia kwa dhamana msanii huyo, lakini jaji wa New York akasema abaki gerezani.

Mfalme huyo wa wimbo wa “I Believe I Can Fly” mapema Julai, 2019 alikamatwa kwa mara ya pili na Idara ya Polisi ya New York kwa tuhuma za kuwasafirisha wanawake kwa ajili ya kuwatumikisha kingono. Mara ya kwanza alikamatwa Februari mwaka jana kwa tuhuma za kuhusika na makosa 10 ya ngono.

Kwa mujibu wa tovuti ya CNN, imeeleza kuwa barua ya maombi hayo iliwasilishwa mahakamani hapo na wakili wake Steven Greenberg ilieleza namba mteja wake huyo mwenye miaka 53 yupo katika hatari ya kupata maambuziki hayo.

Barua hiyo ilieleza namna katika gereza la Metropolitan Correctional Center kusivyokuwa na sabuni na sanitaiza za kutosha na watu wengi wanawekwa katika selo ndogo mbili na kuwapo na msongamano ambao ni hatari kipindi hiki. “Katika vyoo na mabafu vya wageni hapa MCC, hakuna sabuni wala karatasi laini za msalani, hivyo inakuwa ngumu kuosha mikono kabla ya kuingia ndani kuona wafungwa na mahabusu”ilisema sehemu ya barua hiyo.

Mei alikamatwa tena na kushtakiwa kwa tuhuma za kuhusika na makosa 11 ukiachilia makosa 13 ya awali ya unyanyasaji wa kingono ambapo kati ya makosa hayo yalikuwemo yanayohusisha kifungo cha hadi miaka 30 jela.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW