Aisee DSTV!

R. Kelly akamatwa tena na polisi mjini Chicago, Atuhumiwa kosa lingine kubwa linalohusu video za ngono

Msanii nguli wa muziki wa R’n’B nchini Marekani, R. Kelly jana Julai 11, 2019 amekamatwa tena na polisi mjini Chicago kwa tuhuma nyingine za kuwaonesha watoto wadogo video za ngono.

R. Kelly

Amri hiyo ya kukamatwa kwa R.  Kelly imetolewa na mahakama mjini Illinois, Hii ni baada ya kuwasilishwa shauri jipya la tuhuma hizo za unyanyasaji kingono.

Jaji Msaidizi wa Mahakama ya Illinois, Joseph D. Fitzpatrick amedai kuwa shauri hilo litajumuishwa na mashauri mengine 13 aliyofunguliwa nguli huyo wa muziki.

Hii ni mara ya pili R. Kelly anakamatwa ndani ya wiki moja, Jumatatu alikamatwa na kisha akaachiwa kwa dhamana Jumanne.

Mpaka sasa R.  Kelly amefunguliwa mashauri 13 yote yakiwa ni ya unyanyasaji kingono.

Leo Ijumaa R. Kelly anatarajiwa kupandishwa kizimbani kusikiliza shauri hilo, Ambalo litatajwa jijini New York.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW