Tupo Nawe

R. Kelly atishia kujiua nyumbani kwake, simu ya dharura yapigwa polisi kutoa taarifa

Msanii nguli wa muziki wa R’n’B nchini Marekani, R. Kelly ametishia kujiua, hii ni baada ya polisi Mjini Chicago kupokea simu ya dharura kutoka kwa mwanamke mmoja ambaye hakujitambulisha jina akiwataka kuwahi upesi nyumbani kwa gwiji huyo wa muziki.

Image result for R kelly suicide
R-Kelly

Polisi mjini Chicago wameeleza kuwa, walivyokea simu hiyo ya dharura. Walikimbia upesi hadi nyumbani kwa R. Kelly ambapo walimkuta Mwanasheria wake na kudai kuwa hakuna chochote kilichotokea kwani R. Kelly ni mzima wa afya.

Simu hiyo pia, iliwataarifu polisi kwamba wanawake watano walionyanyaswa kingono na R. Kelly nao wapo kwenye hatari ya kujiua, jambo ambalo liliwafanya polisi wafike kwenye jengo la Trump Tower ambako wanawake hao wamekwaa kwa muda tangu waanze kusikiliza shauri lao mahakamani mjini Chicago.

Hata hivyo, mtandao wa TMZ umeeleza kuwa uliwasiliana na Mwanasheria wa R. Kelly na kuthibitisha kuwa taarifa hizo ni za uongo aliyepiga simu alikuwa na jambo lake binafsi, kwani masaa mawili kabla ya taarifa hizo alikuwa na mteja wake.

Kwa sasa, R. Kelly yupo nje kwa dhamana na anakabiliwa na kesi 10 ikiwemo tuhuma za unyanyasaji wanawake kingono, ambazo zote amekataa.

Sikiliza sauti ya mwanamke huyo akiripoti polisi kuhusu R. Kelly – http://www.tmz.com/videos/1_qfqkvkb8/

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW