Tupo Nawe

R.Kelly atiwa mbaroni na jeshi la Polisi, kufikishwa mahakamani muda wowote, sakata la unyanyasaji mabinti kingono lamuweka pabaya

Mwanamuziki wa R&B R.Kelly amekamatwa hapo jana usiku baada ya Mahakama ya Chicago kutoa amri ya kukamatwa kwake kufuatia ushahidi mpya kuhusiana na madai aliwadhulumu kimapenzi watoto 3 kati ya miaka 13-17.

Hakimu amechukua hatua baada mkanda wa video kuonesha tukio lililotokea mwaka 1998.

Hapo jana usiku Februari 22, R. Kelly alielekea kwenye kituo cha Polisi jijini Chicago majira ya saa 8:15 p.m baada ya kutolewa kwa maagizo ya kukamatwa kwake kufuatia tuhuma hizo za kingono.

Msemaji wa Polisi, Anthony Guglielmi alieleza muda mfupi baadae kuwa, Kelly amekamatwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumamosi hii.

Sakata la R. Kelly la unyanyasaji mabinti kingono laibuka upya, wanawake wengine wajitokeza

Wakati wa tukio hilo mwanasheria wa msanii huyo, Steve Greenberg aliviambia vyombo vya habari kuwa wanawake hao wanamzushia tu Kelly ili kujitengenezea kipato.

”Kila mwanamke kwenye documentary hii ananyimbo, na sasa wanaenda kuziachia, vitabu ambavyo wanaenda kuviachia, hivyo ndivyo wanavyoenda kufanya kwa sasa, kila mmoja anajaribu kuona ananufaika kupitia R. Kelly,” amesema mwanasheria huyo wa R. Kelly.

Wanawake wengine wawili walijitokeza na madai ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya mwanamuziki wa R&B,R Kelly. Rochelle Washington na Latresa Scaff walizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuwa walipewa kinywaji pamoja na madawa ya kulevya mara baada ya tamasha la mwanamuziki huyo lililofanyika Baltimore miaka ya 1990.

Kelly mwenye umri wa miaka 52, amekuwa akishutumiwa kwa madai ya unyanyasaji wa kingono kwa wanawake kwa miongo kadhaa lakini hakuwahi kukamatwa wala kukiri makosa yake.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW