Radio na Weasel wadakwa kwa kuingiza bidhaa bila kulipia kodi

Maswahiba wa kundi la Goodlyfe na nchini Uganda, Radio na Weasel wiki iliyopita walimakatwa na walinzi kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe baada ya kuingiza bidhaa ambazo zilikuwa hazijalipiwa kodi.

Wawili hao walikuwa wakitokea nchini China wakiwa na suitcase zilizokuwa zimejaa simu, nguo na viatu ambavyo vilikuwa havijakaguliwa kwenye ofisi za custom.

Inadaiwa kuwa wasanii hao waliomba msamaha na kuahidi kutorudia tena na ndipo walipoachiwa.

Hata hivyo walilazimika kulipa faini ya shilingi milioni sita za Uganda kama nusu ya kodi waliyotakiwa kulipa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents