Burudani ya Michezo Live

Rafael Benitez afunguka mengi kuhusu Manchester United “Naamini itaingia top four, ina kila sifa”

Aliyekuwa kocha wa Liverpool, Real Madrid, Chelsea, Napoli na nyinginezo ila kwa sasa akikinoa kikosi cha Newcastle United, Rafael Benitez amefunguka mengi kuhusu United.

Kocha huyo ameongea hayo kabla ya mchezo wao wa leo usiku ambapo Newcastle wataikaribisha Manchester katika mchezo huo wa ligi.

Benitez amefunguka na kutoa maoni yake kuhusu Manchester na kusema kuwa ” Ni moja ya timu ambayo ni rahisi sana kuingia top four, ni rahisi sana, ni timu ambayo inalinganishwa kwa sasa na Manchester city, Liverpool, na nyinginezo kubwa, tunaongelea moja ya timu kubwa sana duniani kwa kila sifa”

” Wachezaji iliyonayo ni wazuri mno, ni kati timu ambayo ukicheza nayo na ukitaka kushinda itabidi ujipange sana, “Ikiwa tunafanya kazi kwa bidii kama tulivyofanya dhidi ya Watford tunaweza kushindana dhidi ya mtu yeyote lakini unahitaji bahati kidogo,” alisema Mhispania.

“Ikiwa tunataka kushinda dhidi ya Manchester United, tunahitaji kufanya kama Jumamosi kwa juhudi za timu. Unapaswa kuwa bora kwenye mpira na zaidi sahihi katika safu ya mwisho.”

By Ally Juma.Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW