Michezo

Rafael Benitez aipaisha Newcastle mpaka EPL

Kocha Rafael Benitez wa klabu ya soka ya Newcastle United, amefanikiwa kuirejesha tena timu hiyo kwenye ligi kuu ya Uingereza kwa msimu ujao.

Timu hiyo imefanikiwa kufuzu kucheza ligi hiyo kutoka Championship baada ya kufanikiwa kuichapa Preston kwa magoli 4-1 katika uwanja wa St James’ Park.

Magoli ya Newcastle yalifungwa na Ayoze Perez aliyefunga mara mbili, Christian Atsu, Matt Ritchie na goli la kufutia machozi la Preston lilifungwa na Jordan Hugill.

Timu nyingine ambayo ilipanda daraja ni Brighton ambayo ndio inayoongoza ligi kuu ya daraja la kwanza nchini humo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents