Michezo
Rafael Benitez atangazwa kuwa kocha mpya wa Real Madrid
Baada ya kumtimua kocha wake Carlo Ancelotti, klabu ya Real Madrid sasa imemthibitisha ramsi Rafael Benitez kama kocha wake mpya, zikiwa ni siku mbili tu tangu kocha huyo aachane na klabu yake ya zamani, Napoli
Madrid imethibitisha Benitez ametia saini mkataba wa miaka mitatu na ataanza kazi yake mara tu baada ya mapumziko baada ya msimu wa ligi za soka barani ulaya kumalizika.
Benitez aliwahi kuzifundisha timu timu kama Valencia, Liverpool, Inter Milan, Chelsea na Napoli.