Michezo

Rafael Nadal ajitoa Australian Open 2018

Mcheza tenesi namba boja kwa ubora duniani Rafael Nadal wa Hispania amejiondoa katika mashindano ya Australian Open 2018.

Nadal amejiondoa katika michuano hiyo kutokana na kuumia mguu wake wa kulia wakati akicheza na mpinzani wake Marin Cilic.

Mpaka wakati Nadal anajitoa kati kati ya mchezo huo, Cilic alikuwa anaongoza kwa seti 3-6, 6-3, 6-7 (5), 6-2, 2-0.

Kwa hiyo Cilic ametinga nusu fainali yake ya kwanza ya michuano hiyo ambapo atachuana na Muingereza Kyle Edmund.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents