Michezo

Rafael Nadal atakiwa kulipwa shilingi 26m na waziri wa zamani Ufaransa

Mahakama ya nchini Ufaransa Alhamisi hii imeamuru waziri wa zamani wa afya na michezo kulipa nyota wa mchezo wa tenisi Rafael Nadal kiasi cha dola 11,800 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 26 za kitanzania.

Nadal ametakiwa kulipwa kiasi hicho na waziri huyo Roselyne Bachelot kutokana na kuwahi kumtuhumu kutumia dawa zilizokataliwa michezoni.

Roselyne Bachelot ambaye aliwahi kuwa waziri wa afya na michezo kati ya mwaka 2007 hadi 2010, alitoa tuhuma hizo kwa mshindi huyo wa mataji 16 ya grand slam, kupitia runinga Machi 2016 huko Ufaransa.

Nadal alimfungulia mashitaka waziri huyo wa zamani kwa kauli yake hiyo kwa kusema imemuharibia taswira yake kwa jamii na alikuwa akitaka alipwe kiasi cha dola laki moja ambazo ni sawa na shilingi milioni 224 za kitanzania.

Wakati huo huo mchezaji huyo bingwa namba moja ulimwenguni amesema, atatumia fedha hizo kwa ajili ya kuwasaidia watu wasiojiweza nchini Ufaransa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents