Michezo

Rafael Nadal atinga fainali michuano ya China Open

Mchezaji tenis namba moja katika viwango vya ubora duniani, Rafael Nadal amefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya wazi ya China ‘China Open’ baada ya kumfunga Grigor Dimitrov.

Rafael Nadal ametinga mara nne katika michuano ya China Open lakini ameshindwa kuchukua ubingwa huo tangu mwaka 2005

Baada ya ushindi huo Nadal sasa anatarajia kukutana na Nick Kyrgios au Alexander Zverev katika hatua ya fainali baada ya kumfunga Dimitrov leo siku ya Jumamosi.

Katika michezo ya leo ya nusu fainali ya michuano ya wazi ya China, Nadal alicheza na Dimitrov wakati Zverev akicheza na Nick Kyrgios.

Nadal amemshinda mpinzani wake Dimitrov kwa jumla ya seti 6-3 4-6 6-1 na kutinga fainali yake ya 110 tangu kuanza kwake mchezo wa tenis na wa nne kwa michuano ya Beijing.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents