Michezo

Rafael Nadal bingwa mpya michuano ya China Open

Mchezaji tenis namba moja katika viwango vya ubora duniani, Rafael Nadal amefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya wazi ya China ‘China Open’ baada ya kumfunga Nick Kyrgios.

Nadal ametwaa ubingwa huo Jijini Beijing baada ya kumfunga mpinzani wake raia wa Australia Nick Kyrgios kwa jumla ya seti 6-2 6-1.

Rafael Nadal atinga fainali michuano ya China Open

Bingwa wa  michuano ya wazi ya Ufaransa na Mareka, Nadal ameshinda jumla ya michezo tisa na kutwaa taji hilo ambalo amara ya mwisho akiwa amechukua mwaka 2005.

Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 31 hakuna wa kumsimamisha katika mchezo huo kwakuwa anazidi kufanya vizuri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents