Michezo

Rafiki wa karibu wa Cristiano Ronaldo ahakumiwa jela miaka 2

Badr Hari ambaye ni bingwa wa mchezo wa kickboxer mwenye umri wa miaka 32, amehukumiwa kwenda jela miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya shambulizi.

Hari ambaye ni raia wa Morocco aliwahi kuzushiwa kuwa kwenye mahusiano ya jinsia moja dhidi ya mwanasoka bora duniani Cristiano Ronaldo anayekipiga Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno.

Hukumu hiyo ya Hari imetolewa nchini Uholanzi, hivyo atalazimika kutoka kwao Morocco kwenda jijini Amsterdam kutumikia kifungo chake.

Hukumu inasema hakutakuwa na rufaa hadi atakapotumikia kifungo kwa miezi sita kwanza, baada ya hapo ndiyo mwanasheria wake anaweza kuifikisha rufaa sehemu husika.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents