Rage anataka wadhifa wake

RageAliyekuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), Aden Rage amekata rufaa akipinga uamuzi wa Mkutano Mkuu wa TFF kutomrejesha kwenye wadhifa wake


 



Rage


 


Aliyekuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), Aden Rage amekata rufaa akipinga uamuzi wa Mkutano Mkuu wa TFF kutomrejesha kwenye wadhifa wake licha ya Mahakama ya Rufani kutengua hukumu iliyomtia hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela mwaka 2005.


 


Rage alitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo jela na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Februari 23 mwaka 2005 katika kesi ya tuhuma za wizi wa fedha na mali za Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT-sasa TFF) zenye thamani ya sh. milioni 42 iliyokuwa ikimkabili yeye na wenzake watatu.


 


Lakini Rage tangu Desemba 2005 aliachiwa huru kwa msamaha wa Rais, ingawa bado aliendelea na rufani yake akidai alitaka mahakama imsafishe.


 


Hivi karibuni Mahakama ya Rufaa Tanzania ilimwachia huru Rage baada ya kukubaliana na rufani yake.


 


Pamoja na kushinda rufani hiyo TFF ilisema kwa sasa hawezi kurejea kwenye nafasi yake kwa vile katiba ya shirikisho hilo inambana.


 


TFF ilisema Rage anaweza kurejea madarakani kama ataomba nafasi hiyo kwenye uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu, uamuzi ambao uliafikiwa na Mkutano Mkuu wa shirikisho hilo mwezi uliopita.


 


Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa TFF, Florian Kaijage, alisema Rage amekata rufani kwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kupinga uamuzi wa mkutano huo kutomrejesha kwenye wadhifa wake.


 


Kwa mujibu wa Kaijage kikao cha Kamati ya Nidhamu kitafanyika Aprili 20 mwaka huu kujadili rufani hiyo.


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents