Habari

“Raha Ya Muziki Upate Pesa” Richard Mangostino

MangustinoNi wachache sana wanaomjua msanii Richard Mangoustino kama Mwalimu wa muziki katika nyumba ya kukuzia vipaji hapa nchini nya THT ambayo mpaka sasa imeshaonesha umuhimu wake

Mangustino


Ni wachache sana wanaomjua msanii Richard Mangoustino kama Mwalimu wa muziki katika nyumba ya kukuzia vipaji hapa nchini nya THT ambayo mpaka sasa imeshaonesha umuhimu wake kwa kuwatoa wasanii kibao na kuwaweka katika ramani ya muziki hapa nchini.


“nimekuwa mwanamuziki kwa takriban miaka 16 na sita sasa naamini nina uwezo mkubwa sana kimuziki hivyo nikaona sina budi kutumia kile ninachokifamu na kweli nayaona matunda ya kazi yangu kwani waliotumia muda wao kusikiliza ninachowafundisha hivi sasa wamepiga hatua nzuri tu kimuziki” alisema Mzaire hiyu.


Mangoustino amewatoa wasanii kibao ambao wanafanya vizuri sana katika gemu akiwepo Hafsa Kazinja, Mwasiti, Bui bui, Vumi na wengineo kibao ambao wametoka na walio njiani kutoka kisanii na kuzinadi kazi zao.


Pamoja na kuwa Mwalimu wa muziki THT pia anafanya shughuli zake kama msanii na hivi karibuni amechomoka na singo yake inayokwenda kwa jina la ‘Alolo’ ikiwa katika mahadhi ya Rhumba na kuimba kwa lugha ya kizaire akiwa amerekodia studio 69 chini ya prodyuza Mwanx ‘Dah Jamaa ni mkali sio siri’


“Hivi sasa naandaa albam yanu ambayo natarajia kuikamilisha na kuitoa mwishoni mwa mwezi wa tisa na natarajia itakuwa na mchanganyiko wa mahadhi ya tofauti ikiwemo Rhumba, Charanga, Zouk na mangoma kibao ya kiafrika” alisema Mangoustino.


Lengo lake hasa ni kuwa Mwanamuziki wa kimataifa na kuhakikisha analeta mabadiliko makubwa sana kwa wasanii ambao anawafundisha kwani anaamini hao ndio watakaoshilika jahazi la muziki hapa nchini “yote tisa, kumi nataka kuwa na pesa kwanza kwani raha ya muziki upate pesa” alimaliza Mangoustino ambaye ni mzaire mwenye afadhali kwenye kwenye upande wa lafudhi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents