Michezo
Raheem Sterling asajiliwa rasmi Manchester City
Mchezaji wa kimataifa wa Uingereza, Raheem Sterling amejiunga na Manchester City. Alifanyiwa vipimo vya afya mapema Jumanne. Sterling amekamilisha uhamisho wake wa pound milioni 49 kwenda Manchester City akitokea Liverpool.
Winga huyo atavaa jezi nambari 7, iliyokuwa ikivaliwa na James Milner.
Sterling, 20 atakuwa analipwa mshahara wa pound 180,000 kwa wiki. Atajiandaa na City wiki hii kwaajili ya mechi za kujiandaa na msimu mpya.