Habari

Raia wa Kimarekani auawa na kabila hili la ajabu linaloogopeka zaidi India

Mmarekani mmoja ameripotiwa kuuwawa na kabila ambalo linaogopeka nchini India la Andaman na kisiwa cha Nicobar.

Wavuvi ambao walimuokoa walimchukua mpaka kaskazini mwa Sentinel na wanasema, msemaji wa kabila la watu hao alimpiga kwa mkuki katika upande wake wa kushoto akiwa katika maeneo ya ufukwe.

Vyombo vya habari vya nchini humo walisema kwamba alikuwa na kazi maalamu ya kueneza neno la Mungu.

Ni kinyume na sheria kwa wageni kuwasiliana na makabila ya Andaman ambayo yamejitenga na ulimwengu.

Idadi ya watu hao inakadiriwa kuwa 50 mpaka 150.

Wavuvi saba walikamatwa kwa kosa la uvuvi haramu katika kisiwa hicho, polisi walithibitisha.

Vyombo vya habari vya nchini humo vimeripoti pia kuwa mmarekani huyo alikuwa anataka kuwaubiria ukristo watu wa kabila hilo.

Polisi wanasema kwamba Chau aiwahi kutembelea eneo hilo kabla kama mara nne au mara tano akisaidiwa na wavuvi .

Mwanaume huyo alitambulika kwa jina la John Allen Chau

Idadi ya watu wanaoishi katika ukanda huo wa kaskazini wa kabila la Andaman ni ndogo, hawaelewi hata namna ya kutumia ela.Vilevile ni hatia kwa mtu kuwa na mawasiliano na watu hao.

Mwaka 2017, serikali ya India ilisema kuwa mtu kupiga picha au kutengeneza video ya watu wenye asili ya kabila la Andaman ,watahukumiwa kwa kuwekwa gerezani kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.

Mara ya kwanza kabila hili la ‘Sentinelese’ lilianza kusikika mwaka 2004 mara baada ya maafa ya Tsunamikatika bahari ya hindi.

Siku chache baadaye mamlaka ilitangaza katika mkutano na waandishi wa habari kuwa mtu mmoja wa kabila lililotengwa amepona.

Ndege ya jeshi iliyokuwa ikizunguka katika eneo la kaskazini la kisiwa cha Sentinel ilipita katika eneo hilo ili kuwaangalia.

Lakini wakati ndege hiyo aina ya helkopta ilipokuwa inakaribia, watu wa kabila hilo walianza kurusha mishale kwa wanajeshi hao.

“Na hivyo tulibaini kuwa wako salama” rubani alituambia.

‘Sentinelese’ wanatajwa kuwa ni kabila hatari zaidi duniani. Ni miongoni mwa watu wa kwanza ambao walifanikiwa kuhama kutoka Afrika na wanasayansi wanaamini kuwa walikuja katika kisiwa cha Andaman miaka 60,000 iliyopita.

Mwaka 2006, kikundi cha kampeni ya uokoaji watu kimataifa walisema kabila hilo liliuwa wavuvi wawili ambao walikuwa wanajaribu kuingia katika kisiwa chao kinyume na sheria.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents