Habari

Raia wenye hasira wagoma kushiriki uchaguzi mkuu Afrika Kusini, Wadai hawaoni chama kisafi cha kupigia kura

Ikiwa zimebaki siku 20 wananchi wa Afrika Kusini kupiga kura kumchagua rais mpya, wakazi wa vitongoji wenye maisha duni, wamegoma kushiriki kwenye uchaguzi mkuu nchini humo kwa kile walichodai kuwa hawana imani tena na vyama vya siasa nchini humo.

Mapema mwezi huu wakazi wa kitongoji kimojawapo cha Johannesburg cha Alexandra, waliandamana wakilalamika juu ya maisha mabaya na kusema hawatoshiriki kwenye uchaguzi Mei 8, 2019.

Wakati huohuo Rais wa taifa hilo, Cyril Ramaphosa anaegombea muhula wake wa kwanza anaahidi mageuzi makubwa.Rais Ramaphosa

Rais Cyril Ramaphosa anasisitiza kuwa “Ni lazima tujibu machungu na maisha magumu wanaoshuhudia watu wetu hapa. Hata hivyo wakazi wengi hapo hawaamini mambo yatabadilika.“.

Chama cha ANC kilichoko madarakani tangu uhuru wa Afrika Kusini 1994, kina viti 249 sawa na asilimia 62 ya viti 400 vya bunge. Wakati Chama kikuu cha upinzani cha DA kina asilimia 22.

Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa bado chama cha ANC kinaamini kuwa upinzani sio tishio kwa chama tawala.

Wakati kampeni zikipamba moto kabla ya uchaguzi wa Mei 8, 2019, wakazi wengi wa Alexandra hawana imani tena na chama tawala cha African National Congress na wengine hawana pia imani na chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance kilichochukua udhibiti wa jiji la Johanesburg tangu 2016.

Akizungumza na Shirika la Habari la Sauti ya Amerika, Johanna Ditsela mkazi wa kitongoji hicho anasema huwenda hatopiga kura.

Mimi ninahitaji kazi na ninahitaji nyumba kwa ajili ya watoto wangu , ili niweze kuwalea katika nyumba yenye hadhi nilikuwa na matumaini kwamba siku moja nitakapofariki nitawaachia wanangu makazi ya heshima,” amesema Ditsela .

Ditsela mwenye umri wa takriban miaka 50 ameishi katika kitongoji cha Alexandria kwa miaka 30 katika nyumba ya mabati pamoja na watoto wake watano kando ya mtaro wa maji machafu.

NontsikeleloThinto mkazi mwengine wa kitongoji hicho anasema hata Ramaphosa akiwatembelea hatoweza kuleta mabadiliko yeyote

Anaeleza kuwa, “Ramaphosa inabidi atuambie kile tunachotakiwa kufanya. Angalia mahali ninapoishi. Hiki ni kibanda cha chumba kimoja na ninaishi na watoto wangu . kwa mfano mtoto moja akitaka kukoga inatulazimu tutoke nje, mumewangu akikoga watoto wanatoka nje. Maisha gani haya na sote hatuna kazi.Juhudi za Ramaphosa

Rais Ramaphosa amekuwa akihudhuria kampeni usiku na mchana kuwarai wapiga kura milioni 27 kumpatia nafasi nyingine na kukichagua chama chake cha ANC.

Katika kampeni zake kiongozi huyo aliyechukuwa madaraka baada ya aliyemtangulia Jacob Zuma kujiuzulu, kutokana na kashfa za rushwa mwaka 2018, amekuwa akiahidi nyumba mpya, kompyuta mashuleni na maisha bora.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents