Habari

Raia wenye hasira waushambulia kwa mawe msafara wa Rais Museveni, Mbunge wa upinzani ‘Bobi Wine’ akamatwa kwa uchochezi

Msafara wa Rais wa Uganda, Yowel Musevani jana Agosti 13, 2018 mjini Arua umeingiwa na dosari baada ya moja ya gari lililokuwa kwenye msafara huo kubondwa na mawe.

Image result for museveni
Yowel Museveni

Vyombo vya habari nchini Uganda vimeripoti kuwa vurugu hizo zilizuka baada ya askari polisi kuanza kuwafyatulia risasi mamia ya watu waliokuwa wakiandamana kupinga kitendo cha polisi mjini Arua kumpiga risasi Dereva wa Mbunge wa Upinzani, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine.

Jeshi la Polisi mjini Arua kupitia kwa msemaji wake, Emilian Kayema amethibitisha taarifa hizo na kudai kuwa watu kadhaa wanashikiliwa na polisi akiwemo Bobi Wine.

Hata hivyo jeshi hilo limekataa kuweka bayana kama watu hao ni miongoni mwa waandishi wa habari ambao nao usiku wa jana walikamatwa na kupelekwa kusikojulikana hadi hivi sasa.

Rapa Bobi Wine ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kyyadondo yupo mjini Arua kumpigia kampeni rafiki yake  anayegombania Ubunge kwa mwavuli wa vyama vya upinzani, ambapo jana pia Rais Museveni alienda huko kumnadi mgombea ubunge wa chama chake.

Chanzo: Reuters

Related Articles

3 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents