Habari

Raila Odinga akataliwa kupewa passport mpya na idara ya uhamiaji Kenya ili kupisha uchunguzi juu ya safari zake za nje

Aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Amolo Odinga amekataliwa kupewa passport mpya na idara ya uhamiaji wa Kenya Jumanne (June 24) baada ya ile iliyopita kuibiwa.

Odinga and Obama

Mtandao wa Daily Post wa Kenya umeripoti kuwa Ombi la bwana Odinga kupewa passport mpya ilikataliwa na viongozi wa ofisi ya uhamiaji Kenya Jumanne (June 24), baada ya viongozi wa Usalama wa Taifa Kenya (NSIS) kumuamuru Odinga kusubiri kwa wiki kadhaa ili kupisha uchunguzi juu shughuli ambazo amekuwa akizifanya nje ya nchi siku za hivi karibuni.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Idara ya Usalama wa Taifa ya Kenya inafanya uchunguzi juu ya kile alichokuwa anakifanya bwana Odinga katika ziara yake ya Marekani mapema mwezi huu.

Viongozi hao wa idara ya usalama wa taifa wamemwambia bwana Odinga asubiri wiki kadhaa ili ripoti ya uchunguzi huo ikamilike na kukabidhiwa kwa idara ya uhamiaji ili uataratibu wa kupata pasipoti mpya uweze kuendelea.

Waziri mkuu huyo wa zamani wa Kenya alilazimika kuomba hati mpya ya kusafiria baada ya ile ya zamani kupotea pamoja na nyaraka zake muhimu Jumatatu usiku (June 23) baada ya ofisi zake za Raila Odinga Center zilizoko Nairobi, Kenya kuvamiwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents