Habari

Raila Odinga asusia tarehe ya uchaguzi nchini Kenya

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga ametangaza kuwa hayuko tayari kushiriki marudio ya uchaguzi mkuu wa urais nchini humo endapo hakutafanyika mabadiliko kwenye Tume ya Uchaguzi nchini humo.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga

Bwana Odinga amesema kuwa anataka kuwepo mikakati ya kisheria na kikatiba inayohitajika, kabla ya yeye kukubali kushiriki uchaguzi huo utakaofanyika tarehe 17 Octoba mwaka huu.

Odinga anapendekeza Tume ya Uchaguzi nchini humo, ambayo imelaumiwa na mahakama ya juu kwa kuendesha uchaguzi kwa njia ambayo haiukuwa ya haki.

SOMA ZAIDI – Tarehe ya kurudia uchaguzi nchini Kenya yatajwa

Jana Jumatatu Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Kenya ilitangaza kwamba uchaguzi mpya wa urais nchini humo utafanyika tarehe 17 Oktoba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents