Habari

Raila Odinga awashinikiza wafuasi wa upinzani kugoma kwenda kazini

Kiongozi wa vyama vya muungano wa upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Odinga amewashauri wafuasi wake kususia kazi kuanzia kesho jumatatu Agosti 14 kama njia ya kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika jumanne ya Agosti 8.

Tokeo la picha la raila odinga
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga

Akihutubia wafuasi wake huko Kibera jijini Nairobi kwa mara ya kwanza tangu yatangazwe matokeo ya uchaguzi mkuu ambapo Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi, Bw Odinga amedai kuwa serikali ilikiwa imepanga kuwaua wafuasi wa upinzani hata kabla ya matokeo kutangazwa.

Kauli hiyo inakuja baada ya watu 24 kuripotiwa kuuawa maeneo tofauti ya jiji la Nairobi na Kisumu, wakati wafuasi wa upinzani walipojitokeza kulalamikia matokeo ya uchaguzi.

Hata hivyo, Odinga amesema kuwa siku ya Jumanne, Muungano wa vyama vya upinzani (NASA) utatangaza muelekeo wao kuhusu matokeo hayo ya uchaguzi.

Katika kutafuta suluhisho aliyewahi kuwa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Kofi Annan, ambaye alikuwa mpatanishi mkuu baada ya mzozo wa kisiasa nchini Kenya miaka kumi iliyopita, ametoa wito kwa Bw Odinga kutumia mifumo ya kisheria kutafuta haki kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents