Habari

Rais Adam Barrow arudi Gambia kuliongoza taifa lake

Rais mpya wa Gambia Adama Barrow, amewasili nchini humo kuchukua hatamu za uongozi, kufuatia kuondoka madarakani kwa rais wa mda mrefu Yahya Jammeh

Barrow akilakiwa na baadhi ya wananchi

Barrow aliapishwa wiki iliyopita nchini Senegal wakati viongozi wa kieneo walipokuwa wakimshawishi Jammeh kuondoka madarakani.

Maelfu ya watu walifurika katika barabara za mji mkuu wa Gambia Banjul kumlaki rais huyo mpya.

Taarifa zinasema Barrow atakaa katika makaazi yake wakati ukaguzi ukifanywa katika ikulu kutambua hatari yoyote kufuatia kuondoka kwa Yahya Jammeh kwenda uhamishoni Guinea ya Ikweta.

Maelfu kadhaa ya wanajeshi wa mataifa ya Afrika magharibi wanasalia Gambia wakati kukiwa na taarifa kuwa wafuasi waovu wa Jammeh wamo miongoni mwa vikosi vya usalama nchini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents