Siasa

Rais awapa shavu wasanii bungeni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete jana alasiri amesifia tasnia ya muziki filamu na maigizo katika hotuba yake wakati akilihutubia taifa katika hotuba yake ya kwanza ya kufungua bunge la 10.

Bunge hilo ambalo ndio limefunguliwa rasmi kwa mara ya kwanza tangu Rais huyo kushinda uchaguzi uliofanyika mapema mwezi uliopita,ili kuendelea na awamu ya pili ya uongozi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi kwa mwaka 2010-2015.

Akiongelea vipaumbele vya serikali yake ya awamu ya nne, kwa nyanja ya pili ya uongozi Mheshimiwa Rais pamoja na mambo mengine alisema amefarijika sana kuona maendelo ya tasnia za Sanaa ya muziki filamu na maigizo kwa kipindi alichokaa madarakani.

Akionyesha kutoa mfano wa wasanii anaowaona kama wameingia kuleta mwamko na kukuza tasnia ya taarabu kama muziki wa kizazi kipya Mheshimiwa Kikwete alisema kuna msanii anayeitwa Mzee Yusuf ambaye anaona anakubalika sana na wanajamii.

Vile vile katika kuongezea mheshimiwa Rais alisema amefurahishwa na ukuaji wa tasnia ya filamu ambapo alibainisha kuwa huangalia muvi katika kituo cha luninga cha African Magic wakati wa mapumziko yake na alivutiwa zaidi baada ya kuona filamu ya Kiswahili ikionyeshwa katika stesheni hiyo.

Pia alichukua fursa hiyo kuwapongeza origino komedi na wanamaigizo wengine ambao anaona wamepiga hatua kubwa.

Kazi kwenu wasanii kutumia fursa hiyo kumfikishia salamu za ukweli mheshimiwa rais katika ngwe yake ya mwisho ya uongozi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents