Habari

Rais Donald Trump amkosoa Rais wa Ufaransa Macron kuhusu pendekezo lake la kuundwa kwa jeshi la Umoja wa Ulaya

Rais Donald Trump amkosoa Rais wa Ufaransa Macron kuhusu pendekezo lake la kuundwa kwa jeshi la Umoja wa Ulaya

Rais wa Marekani Donald Trump hakupoteza muda kumkosoa mwenyeji wake wa Ufaransa wakati alipowasili Paris kwa ajili ya matukio ya kuadhimisha kumbukumbuku ya miaka 100 ya kumalizika Vita Vikuu Vya Kwanza vya Dunia. Trump aliandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter wakati alitua Paris, akisema kuwa Rais Emmanuel Macron ametoa pendekezo aliloliita kuwa ni “matusi” la kuunda jeshi la Ulaya ili kupambana na Marekani, China na Urusi.

Ilikuwa dalili ya wazi kuwa rais huyo anayeendeleza sera ya “Marekani Kwanza” yuko tayari kuufuata mkondo wake kwa mara nyingine tena wakati viongozi wa dunia wakikutana kukumbuka muungano ulioweka kikomo vita vya kwanza vya dunia.

Kwa mujibu wa DW Swahili, Trump anapanga kukutana na Macron Jumamosi kwa mazungumzo kuhusu mada tofauti yanayotarajiwa kujumuisha usalama wa Ulaya, Syria na Iran. Wakati aliwasili, Trump aliandika kwenye Twitter kuwa Macron “amependekeza kuwa Ulaya iunde jeshi lake ili kujilinda dhidi ya Marekani, China na Urusi. Ni matusi makubwa, lakini pengine Ulaya kwanza inapaswa kutoa mchango wake katika NATO, ambao Marekani inagharamia pakubwa!”.

Ziara fupi ya Trump Ulaya inakuja wakati kukiwa na sintofahamu kuhusu mahusiano kati ya Marekani na bara hilo. Trump kila mara analalamika kuhusu mikataba ya kibiashara na Umoja wa Ulaya na kukosoa baadhi ya mataifa ya Umoja wa UIaya, ikiwemo Ufaransa, kwa kutotoa mchango wa kutoshawa bajeti ya ulinzi ili kuiendeleza jumuiya ya NATO

Katika kumbukumbu ya kesho Jumapili ya kumalizika Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia, Trump atajiunga na viongozi wa dunia katika sherehe zitakazoandaliwa katika lango la Arc de Triomphe. Rais huyo pamoja na mkewe Melania Trump wanatarajiwa kuzuru maeneo kadhaa ya kumbukumbu nchini Ufaransa ambayo yalijengwa kwa ajili ya wanajeshi wa Marekani.

Kuanzia leo Novemba kumi, rais Macron amepanga kukutana na kansela Angela Merkel katika mji wa kaskazini mwa Paris wa Compiègne kwa kumbukumbu fupi. Eneo hilo lina kumbukumbu mbili. Katika toto moja la treni ndiko makubaliano ya kuweka chini silaha yalipotiwa saini November 11 mwaka 1918 kati ya madola yaliyoshinda vita na utawala wa zamani wa Ujerumani reich.

Miaka 22 baadae, baada ya kuivamia Ufaransa, Adolf Hitler akawalazimisha viongozi wa kijeshi wa nchi hiyo wasalimu amri na mkataba kutiwa saini ndani ya toto hilo hilo la treni. Serikali ya Ufaransa lakini inataka kukumbuka tukio jengine la kihistoria: “Tunataka kufuata nyayo za Helmut Kohl na Francois Mitterand walipoingia Verdun mwaka 1984.

“Kwa mujibu wa duru kutoka ikulu ya Ufaransa mjini Paris-Elysée. Tukio la kupeana mikono kansela wa wakati ule wa Ujerumani na rais wa wakati ule wa Ufaransa lilisifiwa ulimwenguni kama tukio la suluhu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents