Habari

Rais hataki kubadili miaka 5 kwenda 7 ila wananchi tunataka – Mhe Juma Nkamia

Ikiwa ni wiki chache toka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kusema kwamba hapendezwi na mjadala unaoendelea juu ya kuongeza muda wa urais kutoka miaka 5 hadi 7, Jumatatu hii Mbunge wa jimbo la Mchemba kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), Juma Nkamia, amesema yeye haoni kama ni tatizo kama rais akiamua kuongeza muda wa uongozi kutoka miaka 5 hadi 7.

Mhe. Rais Magufuli

Akiongea katika mahojiano na kituo cha BBC, Mhe. Nkamia amesema sio rais ambaye anataka suala hilo bali wananchi ndio ambao wanaonekana kuwa na shauku na suala hilo pamoja na kupunguza gharaza za uchuguzi kila baada ya miaka 5.

“Nimemsikiliza Mhe Rais na mwenyekiti wa chama changu amesema yeye asingependa na hafurahishi na hilo jambo,” alisema Nkamia. “Mkubwa akishasema wewe wa chini unatafakari lakini mimi nakubaliana na hoja yake. “Lakini sio yeye anayetaka, mimi kwa mtazamo wangu, kazi anazozifanya na wananchi wanavyosema nikipita katika maeneo mengi naona jinsi anavyokubalika,”


Mbunge Juma Nkamia.

Aliongeza,”Siku zote Rais hawezi kusema mimi nataka kuendelea,wale wanaomwangalia utendaji wake wa kazi na kuona anafaa kupewa muda zaidi. Nisema mimi kwamba sisi wananchi, mimi kama Mbunge kwa mujibu wa kanuni na taratibu za bunge, Mhe Rais kubadilisha miaka 5 kwenda 7 sio jambo baya sana, kwa mujibu wa kanuni za bunge, nitazungumza na Mhe Spika, maelekezo ambayo nitapewa na Mhe Spika ndiyo nitakayoyatekeleza,”

Hivi karibuni Mhe Rais akiwa na Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey PolePole alisema hana mpango wa kuongeza muda wa urais kutoka miaka 5 hadi 7 na pia hapendezwi na mijadala inayoendelea juu ya hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents