Uncategorized

Rais Kabila afunguka kuhusu uchaguzi DRC ‘Utakuwa huru na wa haki, sifuatilii yanayosemwa’

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila amesema kuwa uchaguzi wa nchi hiyo utafanyika kwa huru na haki.

Rais Kabila ameyasema hayo kupitia mahojiano yake na Shirika la habari la BBC, na kusema kuwa huwa hapendi kufuatilia yanayosemwa na watu ila ana uhakika tume yao inauzoefu mkubwa.

‘’Nina hakika uchaguzi utakuwa huru na haki, huwa spendi sana kufuatilia yanayosemwa na wengine ila nina uhakika kwamba tume yetu inauzoefu mkubwa sana. Ita hakikisha kwamba uchaguzi utakuwa huru na haki,” amesema Rais Kabila.

Akizungumzia kuhusu ugonjwa wa Ebola wakati huu wa uchaguzi Rais Kabila amesema ”Ikiwa kama kuna mgonjwa mmoja mwenye Ebola akigusa mashine ya kupigia kura inamaana wengine wote wanaweza kuambukizwa huo ugonjwa.’’

‘’Tuendele na uchaguzi ili baada ya uchaguzi tuwe na watu milioni moja ambao wata kuwa na Ebola au tusimamishe tuhakikishe kwamba tunapigana na huo ugonjwa.’’

‘’Kitu ambacho Congo tumeweza kukataa, ni kuambiwa nini chakufanya au kuwa omba omba hilo tumekataa mimi nimeikataa.’’

‘’Congo unayoijua sasa hivi ilikuwa haipo tena, ni Congo ambayo ilikuwa ni vipande  kwahiyo wananchi wa Congo watakumbuka kwamba tuliweza kuunganisha nchi hii na tumeweza kuhakikisha kwamba tumeimarika uchumi wa nchi yetu.’’

Uchaguzi huo mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) unafuatiliwa kwa karibu na Jumuiya ya Kimataifa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents