Habari

Rais Kabila aipa sifa bandari ya Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC), Joseph Kabila ameyasifu mabadiliko yaliyoanza kuonekana katika bandari ya Dar es Salaam, na kuihakikishia Tanzania kuwa itaongeza kasi zaidi ya matumizi ya bandari hiyo.

imgs0989

Kwa mujibu wa Rais John Magufuli, hadi sasa mizigo inayopitia katika bandari hiyo kutoka na kwenda DRC imeongezeka kwa asilimia 10.6 huku biashara baina ya nchi hizo ikiongezeka kutoka shilingi bilioni 23 mwaka 2009 hadi bilioni 396.3 mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais Magufuli, Ikulu Dar es Salaam jana, Rais Kabila alisema nchi yake iko tayari kuendeleza uhusiano wa kiuchumi na kibiashara uliopo baina ya nchi hizo mbili.

“DRC inatumia bandari ya Dar es Salaam kwa kiasi kikubwa kusafirisha mizigo yake, lakini nikiri kuwa miaka iliyopita tulikuwa na matatizo na bandari hii, lakini kwa kweli kwa sasa hali ni tofauti kwani kumekuwa na mabadiliko makubwa ya huduma katika bandari hii yanayotupa moyo,” alisema Rais Kabila.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents