Habari

Rais Kagame amteua mtanzania kuwa waziri wa miundo mbinu wa Rwanda

Rais Paul Kagame wa Rwanda amemteua profesa mwenye asili ya Tanzania, Silas Lwakabamba, kuwa waziri wa miundo mbinu wan chi hiyo.

Prof-Silas-Lwakabamba

Rais Kagame amelibadilisha baraza lake la mawaziri na kuongeza sura mpya miongoni mwao akiwa Prof Lwakabamba, anayetokea Tanzania. Profesa huyo hata hivyo alipewa pia uraia wa Rwanda.

Profesa Lwakabamba alizaliwa na kusomea Tanzania ambapo alichukua masomo ya engineering katika chuo kikuu cha Leeds nchini Uingereza. Alipopata Phd ya Mechanical Engineering,alirejea Tanzania na kuwa mhadhiri katika kitivo cha Engineering kwenye chuo kikuu cha Dar es Salaam miaka 1970.

Kabla ya kuteuliwa kuwa waziri, Profesa Lwakabamba alikuwa mkuu wa chuo kikuu cha taifa cha Rwanda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents