Habari

Rais Kagame amuonya kiongozi wa upinzani aliyemtoa jela wiki iliyopita ‘ukae kimya au urudi Jela’

Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesikitishwa na kauli za kiongozi wa upinzani nchini humo, Victoire Ingabire ambaye alitoka jela wiki iliyopita kwa msamaha wake, aliyedai kuwa ataendelea kupambana dhidi ya serikali ya Rwanda katika kusimamia Demokrasia.

Related image
Rais Paul Kagame

Rais Kagame amesema hayo wakati akihotubia Bunge nchini humo kwenye mkutano wa  kuapishwa kwa wabunge waliochaguliwa hivi karibuni.

Akisita kutaja jina lake amemuonya kiongozi huyo wa upinzani, Victoire Ingabire akisema msamaha alioutoa ndiyo njia aliyochagua ya kuleta amani na kujenga taifa hilo na sio shinikizo kutoka kwa mataifa ya Magharibi.

Kwa upande mwingine, Kagame amewaonya wafungwa wote walioachiwa kwa msamaha wake kuwa wabadilike na kuwa wakimya la sivyo watarudishwa tena jela.

Bi. Victoire Ingabire ni kiongozi wa chama cha FDU, mapema wiki iliyopita baada ya kutoka Jela alimshukuru Rais Kagame kwa msamaha wake, lakini akasisitiza kuwa hakuomba msamaha kwa kuwa hakufanya kosa lolote na kuahidi kuendelea na mapambano yake ya kupigania demokrasia nchini Rwanda.

Bi Ingabire , ambaye ni kutoka kabila la wahutu, alikamatwa na kufungwa baada ya kuhoji ni kwa nini makumbusho ya mauaji ya halaiki nchini Rwanda ya 1994 hayakuhusisha watu wa kabila la Wahutu.

Kwa makosa hayo mwaka 2013 alikutwa na makosa ya uchochezi na kueneza chuki, jambo lililopelekea kufungwa Jela miaka 15.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents