Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Habari

Rais Kenyatta afuata nyayo za Dkt. Kikwete, apingwa na waandishi wa habari na wanaharakati

By  | 

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta leo Mei 16, 2018 amesaini muswada wa matumizi mabaya ya Kompyuta na makosa ya mtandao na kuwa sheria rasmi ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu nchini humo.

Maamuzi hayo ya Kenyatta yamefanyika Ikulu jijini Nairobi mbele ya Makamu wake William Ruto, ambapo wamesema kuwa hatua hiyo itapunguza kama sio kukomesha vitendo vya uhalifu kwenye mitandao ya kijamii.

Sheria hiyo pia itahusisha na waandishi wa habari ambao wataandika habari FEKI ambapo kosa hilo litajumuishwa kwenye baadhi ya vipengele vya makosa ya uhalifu mtandao.

Hatua hiyo ya Kenya inakuja ikiwa ni miaka miwili tangu aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho mwaka 2015 kusaini muswada wa sheria ya makosa ya mtandao.

Soma zaidi – Rais Kikwete aombwa kutoupitisha muswada wa sheria ya makosa ya mtandaoni, 2015

Hata hivyo, Waandishi wa Habari na wanaharakati nchini Kenya wamepinga hatua hiyo ya Rais Kenyatta kwa kudai kuwa hatua hiyo ni kandamizi na inakiuka haki za binadamu.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW