Siasa

Rais Kikwete atembelea Mbagala

Rais Kikwete atembelea Mbagala
Rais Jakaya M. Kikwete jana amefanya ziara na kutembelea kambi ya jeshi iliyopo Mbagala Kizuiani ambapo ghala la silaha lilipuka hapo juzi na kusababisha vifo vya raia 3 na wanajeshi 5, aidha maeneo yaliyotembelewa ni pamoja na Hospitali zote walipolazwa majeruhi wa milipuko hiyo, Muhimbili na halikadhalika Temeke.

Raisi pia ametembelea mtaa na maeneo ya karibu na kambi hiyo akiwafariji raia na wahanga wa
milipuko hiyo.

Akiendelea na ziara hiyo ametembelea kambi yenyewe na kupewa maelezo
na wasimamizi wa shughuli nzima ya tukio. Aidha alishauriwa pia
kutofika baadhi ya maeneo kufuatia hali ilojitokeza ambapo bomu
lingine dogo lililipuka jana majira ya mchana.

Rais Kikwete atembelea Mbagala

Operesheni inaendelea na vipande vya chuma vimeendelea kuokotwa huku
wananchi wakitaadharishwa kutoa taarifa mara tu waonapo vyuma au vitu
wasivyovielewa.

Wananchi pia wameendelea na zoezi la kuandikisha athari walizozipata
na pia kueleza hofu zao juu ya mali zao zilizoaribiwa na kupotea
wakati wa milipuko hiyo.

Maoni ya wananchi mbalimbali waliohojiwa na na vituo mbalimbali vya
habari nchini wamesema kuwa aidha wakati umefika wa wananchi
kutopuuzia amri za kuondoka au kutofanya makazi ya kudumu katika
maeneo ya hatari.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents