Siasa

Rais Kikwete awatolea mfano Diamond na Michael Jackson kama wasanii wenye nidhamu

Rais Jakaya Kikwete amewataka wasanii wa muziki kuwa na nidhamu ya kazi ambayo itawajenga kimaendeleo ya sanaa pamoja na maisha yao na kuwatolea mfano Diamond Platnumz na marehemu Michael Jackson.

IMG_3601

Akizungumza jana kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam katika semina ya fursa, Rais Kikwete alisema wasanii wasipojitambua na kujifunza watakuwa wakilaumu kila siku na kumtolea mfano Michael Jackson aliyeweza kufanikiwa mapaka akawa Mfalme wa Pop.

“Kitu nilichojifunza kutoka kwa Michael ,nidhamu, kwa pale anapopanda kwenye jukwaa ,hakuna masihara,anaingia wimbo moja, anaingia wimbo mwingine,nonstop,kwamba ile ameifanya ni kazi lakini nimekaa nae akasema hivi,’tukishamaliza ile show ya siku ile,siku inayofuata muda tunautumia wote ni kuangalia video ya show yetu ile ya jana, tumekosea wapi,tuboreshe wapi,hatimaye ndio ajira yangu’. Sasa ile nidhamu aliyokuwanayo kwa ile kazi ndio maana akawa King of Pop,” alisema Kikwete.

“Inaitaji nidhamu, lakini leo umeanza shughuli kidogo,unaacha unasema ‘jamani nyinyi endeleeni mimi nakuja’mimi kesho kidogo nina shughuli’. Hautafanikiwa. Baada ya hapo utaona ile shughuli haina maana kwasababu umekosa nidhamu,nidhamu ni kitu kikubwa. Kwahiyo kwanza nikutambua kama nilivyozungumza na kubadili mtazamo.”

Rais Kikwete alidai kuwa Diamond ni miongoni mwa wasinii wenye nidhamu ya kazi ndio maana hata ameweza kufika hapo alipo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents