Habari

Rais Kim Jong Un aanza utekelezaji wa adhabu mpya ya kifo aliyojifunza kwenye filamu ya James Bond, Atakayekutwa na hatia kugeuzwa kitoweo

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un amefanya majaribio ya njia mpya ya adhabu ya kifo kwa kumuadhibu kiongozi mmoja wa jeshi nchini humo aliyedaiwa kupanga jaribio la kuipindua serikali yake.

Kim Jong Un

Adhabu hiyo ya kifo kwa sasa itakuwa ni ya kudumbukizwa kwenye bwawa la samaki wakali aina ya Piranhas ili abaki kuwa kitoweo cha samaki hao.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail limeeleza kuwa adhabu imeanza kutumiwa kwa mara ya kwanza kupitia kwa kiongozi huyo wa jeshi.

Mabwawa hayo ya kisasa (Aquarium) yamejengwa katika makazi ya Rais Kim Jong yaliyopo Ryongsong mjini Pyongyang.

Hata hivyo, kwa mujibu wa picha zilizopigwa na kituo cha runinga cha taifa hilo, zilimuonesha mhukumiwa huyo akihangaika kwenye mabwawa hayo huku akionekana hana mikono na miguu.

Mpango wa adhabu hiyo mpya, imeelezwa kuwa wazo lilitoka katika filamu ya “The spy who loved me” ambapo kwenye filamu hiyo kuna watu wanahukumiwa kwa kudumbukizwa kwenye bwawa la Papa.

Imeripotiwa kuwa tangu Rais Kim aingie madarakani mwaka 2011, ametekeleza adhabu ya vifo kwa watu 16 wakiwemo viongozi 11 wa serikali yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents