Habari

Video: Rais Magufuli aagiza watoa vibali vya sukari wafukuzwe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amempa siku tatu Waziri wa Kilimo, Dkt. Tizeba kuwaondoa mara moja maafisa wote wanaotoa vibali kwa waingizaji wa sukari katika kitengo hicho.

Akizungumza na wananchi wa Missenyi mkoani Kagera alikotembelea kiwanda cha sukari Kagera, Rais Magufuli amesema watu hao wakapangiwe kazi nyingine tofauti na kutoa vibali.

“Kuna watu pale wizara ya kilimo kazi yao ni kutoa vibali tu, na nina fikiri wale uwafukuze wote tu there useless kazi zao ni kutoa vibali ndivyo wamekuwa wakiishi, vibali vya sukari bado wapo hao watu? Wale ukawatoe wahamishie kwingine ambako hawatoagi vibali kama kuna vibali vya chanjo za mbwa wakatoe huko, kila siku ni vibali na vibali ni vya fojari vya ajabu, wanapewa vibali watu wa ajabu hata wale ambao hajawahi kusafirisha hata sukari, alafu wakishapewa wanaenda kuuza vibali wanapewa wengine wanachama wa CCM wengine wa vyama vingine chukua hiki kibali nae anaenda kuuza kwa wale wana supply, na fikiri huo mtindo ni mbaya,” alisema Rais Magufuli.

“Waziri kawatoe wale wote wanaotoaga vibali pale wizarani kwako ndani ya siku 3 kawatoe wapangie kazi nyingine kama walisomea kutoa vibali mbona vipo vibali vingi kama vya kulima haiwezekani wamekaa pale there so specialized na wale ndio special wa kutoa rushwa kwahiyo waziri nakuachia hiyo kazi na wizara wa biashara kasimamie hilo waziri wa kilimo na nini kafanye hiyo kazi tunataka twende mbele mambo ya kudekezana haya na hawa watoa vibali hawawezi kufurahia wakiona vibali vinafanya kazi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents