Habari

Rais Magufuli aeleza sababu za kumteua Prof. Kitila wa ACT- Wazalendo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemwagia sifa Profesa Kitila Mkumbo (ACT Wazalendo), kuwa ni kijana mwenye akili ndiyo sababu iliyomfanya amteue kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Rais Mgufuli amesema hayo leo katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika Uwanja wa Lake Tanganyika ambapo amehutubia wananchi.

“Hongera sana Profesa Mkumbo kijana safi, sura yako ni ACTwazalendo lakini moyo wako ni CCM.  Watu wanauliza nimemteuaje mtu wa ACT -Wazalendo si nimeona ana akili ndiyo maaa nimemteua,” amesema Rais Magufuli.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents